SSERUNKUMA AKISAINI SIMBA MBELE YA RAIS WA KLABU HIYO, EVANS AVEVA. |
Kamati ya Usajili ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Zacharia Hans Poppe leo imekamilisha usajili wa miaka miwili wa mshambuliaji nyota wa Uganda, Danny Sserunkuma.
Sserunkuma aliyekuwa anakipiga Gor Mahia ya Kenya amekamilisha usajili Simba ikiwa ni baada ya kumaliza mkataba wake na mabingwa hao wa Kenya.
Kabla ya hapo, Mganda huyo alifanyiwa vipimo vya afya jijini Dar, kabla ya usajili wake kufanyika.
0 COMMENTS:
Post a Comment