Straika wa zamani wa Yanga,
Mkenya, Boniface Ambani, amekikubali kiwango cha kiungo mshambuliaji wa timu
hiyo, Mbrazili, Andrey Coutinho, huku akimshauri kuingia gym.
Kauli hiyo, aliitoa
mshambuliaji huyo mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara
iliyowakutanisha Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Ambani ambaye sasa ni mfanyabiashara alisema kuwa kiungo huyo amepungukiwa vitu vichache pekee
ambavyo vinarekebishika kama akihitaji, ambavyo ni nguvu na pumzi ya kutosha.
Ambani alisema, kiungo huyo
anatakiwa kufanya mazoezi yatakayomuongezea vitu hivyo, ikiwemo kuingia gym na
kukimbia ufukweni kwa ajili ya kujiweka fiti.
“Nikwambie ukweli tu, Yanga
wamesajili vizuri sana na hiyo ni kutokana na ubora wa kila mchezaji kwa jinsi
nilivyowaona kwenye mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting ambayo ilimalizika kwa
suluhu.
“Ukiangalia mchezaji kama
yule Mbrazili (Coutinho) ni mzuri ana kiwango kikubwa, lakini ana upungufu
mdogo ambao unarekebishika wa kukosa stamina na nguvu pekee, nikuhakikishie
kama akifanikiwa kuvifanyia kazi vitu hivyo, basi atakuwa tishio, niamini mimi,”
alisema Ambani.
0 COMMENTS:
Post a Comment