Baada ya kuandamwa na
vipigo mfululizo katika ligi kuu, uongozi wa Ndanda FC umeibuka na kuomba
msamaha kwa mashabiki wake.
Timu hiyo wikiendi
iliyopita iliambulia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba, katika uwanja wao
wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona na mpaka sasa ipo nafasi ya pili kutoka mkiani
ikiwa na pointi kumi pekee.
Msemaji wa timu hiyo,
Idrisa Bandari, alisema kuwa si kwamba wao wanapenda kupoteza kila mchezo, bali
ni aina ya matokeo ambayo yanawatokea kama sehemu ya mchezo.
“Mashabiki wetu watusamehe kwa matokeo mabaya, si kwamba
tunapenda kuwa hivyo, timu inajituma sana, tunapata nafasi lakini hatuna bahati
kabisa pia ligi imekuwa ngumu sana kwa sasa.
“Lakini wasikate tamaa,
waendelee kutusapoti kuhakikisha tunapiga na kuweza kufanya vyema ingawa
ushindani unazidi kuwa mgumu,” alisema Bandari.
0 COMMENTS:
Post a Comment