January 26, 2015

 Mshambuliaji Mario Balotelli haishi vituko, sasa amemtema mpenzi wake mwanamitindo Fanny Neguesha.

Kisa cha Balotelli kumtema mwanadada huyo mwanamitindo, eti hapendi apige zile picha dizaini kama zinaonyesha mwili wake sana.

Lakini pia kuna picha ya ‘mijibaba’ ikiwa imemkumbatia, yeye hataki kuamini hiyo ni kazi.

Balotelli alikuwa ameishamvisha pete yenye thamani ya pauni 25,000 lakini inaelezwa Fanny ambaye asili yake ni Nigeria ameisharudisha pete hiyo.

Ukiangalia ukurasa wake wa Instagram, mwanadada huyo anatembea mji mmoja baada ya mwingine na picha ndiyo mambo yake.

Mzee mzima Ballo amesema haiwezekani, dada aliposhikilia msimamo wake, kampiga chini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic