Beki mpya wa Simba, Hassan
Kessy, ameuomba radhi uongozi wa Mtibwa kutokana na rafu mbaya aliyomchezea,
Ibrahim Rajabu ‘Jeba’ katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliozikutanisha timu
hizo hivi karibuni.
Beki huyo kabla ya kutua
Simba alikuwa akiichezea Mtibwa, baada ya kutokea tukio hilo viongozi wa Mtibwa
walikuja juu na kumshutumu kutokana na kitendo hicho ambacho si cha kiungwana.
Kessy alisema rafu ile ni bahati mbaya na kwenye mchezo inatokea,
lakini anaomba asamehewe kwa kitendo kile kwani hana ugomvi na mchezaji huyo.
“Nimeondoka Mtibwa kwa
amani na wala sijawahi kuwa na ugomvi kuanzia kwa viongozi mpaka kwa wachezaji
kwa sababu mpaka naondoka kila kitu kilikuwa sawa.
“Unajua sikupanga kumchezea
rafu Jeba kama inavyotafsiriwa, lakini imetokea bahati mbaya kama sehemu ya mchezo
na tunapaswa kusameheana, sasa nafanya kazi pamoja na Simba, hivyo ninahitaji
Baraka zao ili nijitume na kufanikiwa,” alisema Kessy.







0 COMMENTS:
Post a Comment