Uwezo wa hali ya juu
unaonyeshwa na safu ya ushambuliaji ya Yanga umempa kiwewe Kocha wa Simba, Goran
Kopunovic na kujikuta akisema hawa jamaa ni noma.
Mserbia huyo wa Simba aliyejiunga
na timu hiyo hivi karibuni akichukua mikoba ya Mzambia, Patrick Phiri, amesema
kuwa washambuliaji hao ni hatari na ni watu wa kuchungwa sana katika mashindano
haya.
Ijumaa iliyopita washambuliaji
wa Yanga, Simon Msuva na Kpah Sherman walionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo
huo, huku Msuva akifunga moja na Sherman moja.
Kopunovic alisema tangu ameanza kufuatilia mashindano hayo, Yanga ndiyo wana
washambuliaji bora zaidi.
“Nimejifunza mambo mengi katika mashindano haya na
ninaendelea kujifunza ili niweze kuona tofauti iliyopo kati ya timu yangu na
nyingine zinazoshiriki michuano hii.
“Hata hivyo kuna mambo
ambayo tayari nimeshayaona na nitakuwa nikiyafanyia kazi kidogo kidogo ili
kikosi changu kiweze kuwa bora zaidi, ninaamini nitafanikiwa juu ya hilo.
“Safu hatari ya
ushambuliaji ambayo mpaka sasa imenivutia ni ile ya Yanga, hususani wachezaji
wale waliofunga mabao dhidi ya Jang’ombe (Msuva na Sherman) jamaa ni hatari,”
alisema Kopunovic ambaye pia juzi Jumamosi aliongoza timu yake kupata ushindi
wake wa kwanza katika mashindano haya dhidi ya Mafunzo baada ya kushinda bao
1-0.








0 COMMENTS:
Post a Comment