January 4, 2015


Mshambuliaji Andrey Coutinho ametoa 'nuksi' baada ya kufunga bao lake la kwanza akiichezea Yanga bila ya kuwa na Kocha Marcio Maximo.


Coutinho aliletwa nchini na Maximo ambaye alidumu nchini kwa miezi sita tu kabla ya kutupiwa virago na Yanga.

Akiichezea Yanga chini ya Kocha Hans van der Pluijm, Coutinho ameweza kufunga bao lake la kwanza chini ya kocha huyo pia la kwanza kwa mwaka 2015.

Katika mechi dhidi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Polisi Zanzibar, Coutinho amefunga bao la kwanza kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kabla ya Kpah Sherman raia wa Liberia kufunga la pili.

Hadi mapumziko, Yanga imekwenda ikiwa inaongoza kwa mabao hayo mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic