Kipa wa zamani wa Liverpool, Pepe Reina amesema
naodha wake wa zamani, Steven Gerrard ni bonge la nahodha.
Reina alikuwa kipa wa Liverpool tokea 2005 hadi
2013 Gerrard alikuwa ni nahodha wa kweli.
“Alikuwa kiongozi wa kweli, aliongoza kwa mifano
na si maneno. Kuanzia mazoezini hadi uwanjani.
“Alikuwa ni mtu mwenye heshima ya juu kwa
wachezaji wenzake na huwezi kusikia mtu anamlalamikia,” alisema Reina ambaye
kwa sasa anakipiga Bayern Munich.
Gerrard ametangaza ataachana na Liverpool mwishoni
mwa msimu huu, hali ambayo imezua mjadala mkubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment