Mshambuliaji Asamoh Gyan ameamsha matumaini ya Ghana 'Black Star' baada ya kufunga bao pekee katika dakika tatu za nyongeza.
Gyan amefunga bao hilo katika mechi ya Kundi C katika Kombe la Mataifa Afrika na kuiwezesha Ghana kuitwanga Algeria bao 1-0.
Ushindi huo katika michuano hiyo inayofanyika Equatorial Guinea imeamsha matumaini ya Ghana ambayo haikuwa na pointi baada ya kufungwa katika mechi ya kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya Senegal.
Maana yake Ghana ina pointi tatu sawa na Algeria na Senegal na sasa uhakika wa nani anasonga utapatikana katika mechi ya mwisho lakini Senegal wanaweza kufuzu baadaye kama watashinda dhidi ya Afrika Kusini hapo baadaye leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment