GAZETI LA CHAMPIONI LA LEO IJUMAA... |
Ile picha iliyochapishwa kwenye gazeti la Championi Jumatatu iliyopita imezidi kuzua gumzo.
Picha hiyo ilimuonyesha mshambuliaji wa
Yanga, Amissi Tambwe akipigwa kabali na beki wa Ruvu Shooting, George Michael.
Wadau wengi wamekuwa wakipinga jambo hilo lakini leo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameibuka na kuongeza kupinga ukatili huo wa beki wa Ruvu, lakini akaibua jipya..huku akisema hata
yeye inaonekana alifanya makosa makubwa na alistahili kadi nyekundu.
“Kama umeona ile picha iliyochapishwa kwenye gazeti la Championi leo Ijumaa, inaonyesha wazi kabisa kuwa Tambwe anampiga kibao yule beki wa Ruvu.
"Lakini picha ya leo, inaonyesha hata Tambwe anastahili adhabu na siku ile alitakiwa apewe kadi nyekundu," alisema Hans Poppe.
Picha ya kwanza iliyozua gumzo ni ile
iliyochapishwa kwenye Championi Jumatatu Tambwe akiwa amekabwa lakini Championi
Ijumaa likachapicha picha nyingine ikionyesha Tambwe akijibu mashambulizi kwa
beki huyo wa Ruvu.
Tayari mwamuzi wa mchezo huo wa Yanga dhidi ya
Ruvu Shooting uliomalizika kwa sare ya bila bao Jumamosi iliyopita, Mohamed
Theopili amesimamishwa akisubiri uchunguzi na siku yake ya kujitetea ambayo
imeelezwa itakuwa ni Februari 6.
0 COMMENTS:
Post a Comment