Hatimaye Steven Gerrard ameamua
kufunga na kueleza kilichochangia yeye kutangaza kuondoka Liverpool.
Gerrard ,34, kipenzi cha
mashabiki wa mashabiki wa Liverpool ametangaza kuondoka mwishoni kwa msimu.
Akizungumza katika
mahojiano na runinga ya klabu hiyo, Gerrard amesema alipoitwa na kocha Brendan
Rodgers na kuambiwa wakati uliwadia wa kufuatilia kwa karibu uchezaji wake.
Baadaye alianza kutokea
benchi, jambo ambalo aliamini ilikuwa ni sawa na kauli ya mafumbo, kwamba
nafasi yake ni finyu.
“Naelewa, ila ulikuwa ni uamuzi mgumu sana. Nimekuwa
Liverpool muda mwingi. Baada ya mazungumzo yetu nikajua kuna jambo hivyo ni
lazima nilifanyie kazi,” alisema Gerrard.
“Bado nina miezi sita,
nahitaji kujituma na kuisaidia klabu. Nikiondoka, bado siku moja ningependa
tena kurejea.
“Kama nitakuwa kocha au
vinginevyo, ningependa kuja kuendeleza mchango wangu kwa Liverpool,” alisema Gerrard
aliyejiunga na Liverpool akiwa na miaka nane.
0 COMMENTS:
Post a Comment