January 10, 2015

STAND ILIYOUSHINDWA MZIKI WA JKT RUVU...
JKT Ruvu imefanikiwa kujiongezea pointi tatu muhimu za Ligi Kuu bara baada ya kuichapa Stand United kwa mabao 2-1.


Katika mechi hiyo iliyomalizika punde kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, ilikuwa tamu na ya kuvutia.

Kocha wa Stand alilazimika kumtoa kipa Mohammed Makaka kutokana na kufungwa mabao 'laini' na nafasi yake ikachukuliwa na John Mwenga.

Mpira wa kwanza alishinda kuumiliki ukampita na ule wa pili alisimama akidhani unatoka, ukajaa wavuni.

JKT walianza kufunga katika dakika ya 18 kupitia Samwel Kamutu, Stand wakasawazisha dakika mbili baadaye Mussa Said na zikaenda mapumziko na mabao hayo.

Shukurani kwa Amos Mgida ambaye alifunga bao la pili katika dakika ya 60 na Stand hawakuweza kulirejesha hadi mwisho wa dakika 90.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic