Vinara wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar wameimeng’oa JKU na
kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Mtibwa imetinga fainali
baada ya kulazimika kuingia kwenye changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya
kumaliza muda wa kawaida kwa sare ya bila kufungana.
Ushindi wa penalti 4-3
ndiyo ulioipeleka Mtibwa Sugar ambayo beki wake David Luhende pekee ndiye
alipoteza mkwaju wake kwa kupiga nje.
Wachezaji wawili wa JKU nao
walipaisha mikwaju yao na kumpa nafasi Vicent Barnabas kuwamaliza.
Sasa Mtibwa inamsubiri
mshindi kati ya Simba dhidi ya Polisi Zanzibar leo usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment