January 23, 2015


Kiungo wa zamani wa Malindi ya Zanzibar, Shaku Kihwelo amefariki dunia baada ya kumwagiwa maji na mtu mmoja aliyetambulika kuwa ni raia wa Zimbabwe.


Kiungo huyo ambaye ni mdogo wa Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo amefariki dunia nchini Afrika Kusini na tayari tayaribu za kuleta mwili wake nchini kwa ajili ya mazishi zimeanza.

Kaka yake mwingine, Mwanamtwa Kihwelo amethibitisha kuhusiana na kifo cha mdogo wake huyo aliyewahi pia kuichezea Twiga FC.

"Kweli alimwagiwa maji na huyo Mzimbabwe ambaye walipishana kauli. Aliungana sana tumboni, juhudi za madaktari hazikuweza kuzaa matunda na ndiyo tumekutana na matatizo hayo.

"Tunatakiwa takribani randi 18,000 ili kuhakikisha mwili unafika nyumbani kwa ajili ya mazishi," alisema Mwanamtwa.

BLOG HII INATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA KIHWELO. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic