January 23, 2015

 

Kinda wa miaka 16 tu, ameamua kuachana na timu kibao zilizokuwa zikimhitaji na kuamua kutua Real Madrid.

Kati ya timu zilizokuwa zikimtaka kinda huyo kwa hali na mali ni Manchester United, Manchester City na Liverpool.

 
Martin Odegaard raia wa Norway ambaye tayari anaichezea timu ya taifa ya nchi hiyo amejiunga na Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni 2.3. Kinda huyo anaanza kazi huku akilipwa kitita cha pauni 40,000.

Kijana huyo amesema alikuwa akivutiwa na mkongwe Zinedine Zidane ambaye amekuwa ushawishi mkubwa sana kwake kujiunga na Real Madrid.

Martin Odegaard ameonekana akiwa katika picha ya pamoja na Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos baada ya kuwasili katika mazoezi ya Real Madrid.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic