January 28, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, amesema kuumia kwa mchezaji wake, Emmanuel Okwi, katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Azam kuliwachanganya.
Katika mchezo huo, Okwi alitolewa uwanjani hapo akiwa hajitambui baada ya kugongwa kichwani na beki wa Azam FC, Aggrey Morris, wakiwa katika harakati za kugombania mpira  ambapo mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.

Akizungumza jijini Dar Kopunovic amesema kuumia kwa mchezaji huyo, kulimfanya yeye pamoja na benchi lake la ufundi kushindwa kufikiria mchezo huo na badala yake kuwaza mchezaji huyo anaendeleaje.

“Nilikuwa na hofu baada ya kuumia kwa Okwi kwa sababu kwanza ni mchezaji nyota ndani ya kikosi chetu, lakini pia ukirudi katika hali ya ubinadamu, afya ya mtu ni muhimu sana kuliko jambo lolote lile.

“Yaani sikuwa katika hali ya kawaida katika dakika kama ishirini za mwisho ambapo hata mchezo wenyewe sikuwa nafuatilia kwa umakini, muda wote nilikuwa nawaza kuhusu afya ya mchezaji wangu,” alisema Kopunovic.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic