January 31, 2015


Mawakala zaidi ya watano wamejitokeza kwa Klabu ya Simba na kuomba kumchukua kiungo wa klabu hiyo, Said Ndemla kwenda kufanya majaribio katika moja za timu za nje, hasa barani Ulaya.


Ikiwa mipango hiyo itakubalika na kwenda inavyotakiwa, maana yake ni kuwa itakuwa mara yake ya kwanza.

Awali, kulitolewa taarifa kuwa, wachezaji wengine wa klabu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Hassan Kessy, walikuwa kwenye mipango ya kwenda kufanya majaribio katika Klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Evans Aveva ambaye ni rais wa Simba ndiye aliyefunguka kila kitu kwa kusema:

“Tunashukuru tunaendelea kutengeneza vijana na wanafanya vizuri, mawakala watano kutoka nje wameanza kuvutiwa na uwezo wa Said Ndemla, mipango inafanyika ili baada ya msimu huu wa ligi kuu kumalizika aweze kwenda nchi tofauti kufanya majaribio.

“Kwenye mchezo wetu na Azam viongozi wa Real Madrid walivutiwa na kiwango cha Singano na Kessy, waliomba CD zao kwenda kuifanyia kazi.

“Ni jambo la kujivunia, zaidi mashabiki wetu waendelee kuisapoti na kuiunga timu mkono ili kuweza kusonga mbele na kufanya vizuri, wasikate tamaa, timu itafanya vema.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic