Straika machachari wa Mtibwa Sugar, Mussa
Hassan Mgosi, amesema hataangalia historia kuwa wameifunga mara ngapi Simba
msimu huu kwa kuwa itamharibia isipokuwa atakwenda kufanya kazi siku hiyo
kuhakikisha wanaifunga Simba kwa mara nyingine na kutwaa ubingwa.
Tangu kuanza kwa msimu huu, Mtibwa imekutana
na Simba mara tatu ambapo imefanikiwa kushinda mara mbili na kutoa sare mara
moja.
Timu hizo sasa zitakutana tena kesho kwa mara
ya nne ndani ya msimu mmoja kwenye fainali hiyo ya Mapinduzi inayotarajiwa
kupigwa usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
“Historia
kwenye soka siku hizi si kitu cha kuzingatiwa sana, kwangu mimi nimeshafuta
hiyo historia na nitaanza upya kwenye dakika 90 za kesho kwa ajili ya
kuhakikisha naisaidia timu yangu ili tushinde katika hiyo fainali na tutwae
ubingwa, kwa kuwa ndicho kilichotuleta huku,” alisema Mgosi.







0 COMMENTS:
Post a Comment