Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, amefanikiwa kuweka rekodi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi
inayomalizika kesho Jumanne visiwani Zanzibar.
Kopunovic aliyechukua mikoba ya Mzambia,
Patrick Phiri aliyeondolewa kukinoa kikosi cha Simba mwishoni mwa mwaka jana,
ameiongoza timu hiyo kushinda michezo minne mfululizo ya Kombe la Mapinduzi,
rekodi ambayo haijafikiwa na kocha yeyote katika michuano hiyo.
Awali Simba ilianza kwa kupokea kichapo cha
bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa wakati kocha huyo akiwa jukwaani akishuhudia huku
kocha msaidizi, Selemani Matola akiwa analiongoza benchi hilo la ufundi.
Baada ya mchezo huo, Kopunovic akaanza kuiongoza
Simba kuifunga Mafunzo bao 1-0 halafu wakapata ushindi kama huo dhidi ya JKU,
michezo yote hiyo ikiwa ni ya makundi.
Katika hatua ya robo fainali wakaitandika
Taifa Jang’ombe mabao 4-0 na juzi Jumamosi wakafanikiwa kuingia fainali kwa
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi ya Zanzibar, kama Simba wakifanikiwa
kuifunga Mtibwa kesho Jumanne kwenye mchezo wa fainali basi kocha huyo atakuwa
amemaliza michuano hiyo akiwa hajapoteza wala kutoa sare mchezo wowote tangu
aanze kuinoa Simba.








0 COMMENTS:
Post a Comment