January 31, 2015


Kocha Mkuu wa Ruvu JKT, Fred Felix Minziro amesema wataonyesha burudani ya kutosha katika mechi yao ya leo dhidi ya Simba.


Minziro amesema anajua Simba watakuwa wamejiandaa baada ya kufungwa katika mechi iliyopita dhidi ya Mbeya City.

“Tunajua Simba watakuwa wamepania kufanya vizuri, lakini hata sisi tunataka kushinda baada ya kumaliza kwa sare katika mechi iliyopita.

“Tumejiandaa na utaona, kwa kuwa tumepanga kushambulia,” alisema Minziro.

Katika mechi ya mwisho timu hizo zilikutana kwenye Uwanja wa Taifa na Simba ikalala kwa mabao 3-2.


Ruvu JKT ina pointi 18 na inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic