Straika wa Yanga, Kpah Sherman, raia wa Liberia,
amefunguka kuwa anahitaji kuwa mchezaji bora katika kikosi cha timu hiyo kwa kukisaidia
kwenye ligi na michuano ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la
Soka Afrika (Caf).
Sherman amesajiliwa Yanga katika usajili wa
dirisha dogo na tangu atue Jangwani kiwango chake kimekuwa kikiwakuna mashabiki.
Sherman
ameeleza kuwa, anajua Yanga wamemuamini ndiyo maana wamemsajili, hivyo kama
mchezaji wa kulipwa, anahitaji kuitumikia ipasavyo timu yake hiyo ili iweze
kufanya vizuri katika ligi na michuano ya kimataifa.
“Mimi
ni mchezaji professional na ninatambua miiko ya mchezaji wa kulipwa, Yanga
imeniamini na imenisajili, hivyo nahitaji kuitumikia kwa nguvu kuhakikisha inafanya
vyema kwenye ligi na michuano ya kimataifa.
“Nitajitahidi kuhakikisha najaribu kuwa bora
katika timu yangu kwa kufanya vyema kwa kujituma uwanjani na sihofii ushindani
wa namba,” alisema Sherman.







0 COMMENTS:
Post a Comment