January 31, 2015


Nahodha wa Simba, Isihaka Hassan amewataka mashabiki kukubali kuungana na timu yao wakati wa shida na raha.

Isihaka ameyasema hayo mara tu baada ya kikosi hicho kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu JKT katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Isihaka amewataka mashabiki wa Simba kuungana nao.

"Vizuri mashabiki wakajua sisi tunahitaji ushindi ndiyo maana tunakuja kupambana hapa uwanjani.

"Si tukifungwa watu waseme ni wachezaji ni wazembe au viongozi wana matatizo. Badala yake wajue tumeteleza na waungane nasi," alisema.

Alisema wanaendelea kujiandaa vema ili waweze kufanya vizuri hadi mwisho wa ligi.

Mabao yote mawili ya Simba katika mechi hiyo, yamefungwa na Danny Sserunkuma ambaye alipokea pasi mbili za Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic