Kocha Patrick Phiri ambaye amefutwa kazi Simba amekumbushia jinsi alivyoacha kazi ya ukocha wa timu ya taifa ya Namibia kuja Simba.
Alisema alipata ofa nzuri kutoka kwa Shirikisho la
Soka Namibia ambapo alikuwa aende kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, lakini
akaamua kuja Simba kutokana na heshima aliyowapa.
Phiri ambaye alitarajia kuondoka jana
amefungishiwa virago kwa kile kilichosemwa kuwa ni kutokana na mwenendo mbovu
wa timu ambapo amefungwa mechi moja tu kati ya nane dhidi ya Kagera Sugar wiki
iliyopita.
Phiri
amesema kuwa kabla ya Simba kumhitaji alikuwa na ofa nzuri nchini Namibia,
lakini aliamua kuja Simba kutokana na kuifahamu vema hivyo isingekuwa kazi
ngumu kwake pia na mapenzi makubwa aliyonayo kwani ameifundisha mara kadhaa.
“Nilikuwa na ofa kule Namibia tena nzuri,
lakini niliamua kuwasikiliza Simba kwa kuwa kwanza ni timu yangu, nimekuwa nao
kwa muda mrefu, pia nilijua ingekuwa kazi rahisi kwangu kwa kuwa si mazingira
mageni kwangu.
“Siwezi kusema kuwa Simba ilikuwa imenishinda
ila wenye maamuzi ni wao (viongozi) wanaojua wapi penye udhaifu katika timu
yao. Nadhani hii ni mara yangu ya tatu kuja Simba kwa hiyo nilijua mambo
yangekuwa rahisi kwangu kutokana na kuifahamu vema,” alisema Mzambia huyo
ambaye alikuwa akikunja kitita cha milioni nane kwa mwezi.
Nafasi yake imechukuliwa na Mserbia, Goran
Kopunovic ambaye kibarua chake cha kwanza kitakuwa kwenye Michuano ya Kombe la
Mapinduzi huku Visiwani Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment