Ili kuhakikisha inawashambulia zaidi wapinzani
kila mara, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, amewapiga marufuku viungo wake
Haruna Niyonzima na Salum Telela kurudisha mipira nyuma wakiwa wanaelekea goli
la wapinzani wao.
Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni jijini Dar
kabla ya kuelekea Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi, linaloendelea visiwani
humo.
Pluijm amesema kuwa viungo wake hao ndiyo waliocheza bila kufuata maelekezo yake
ambayo ni kucheza soka la pasi za haraka na kupiga pasi za nyuma wakati
wanalishambulia goli la wapinzani wao.
Pluijm alisema hilo ameliona na mengine
likiwemo suala la mawasiliano kati ya mabeki na kipa wake jambo lililosababisha
bao la pili la John Bocco.
Aliongeza kuwa, amepanga kuufanyia kazi upungufu
aliouona kwenye mechi za Kombe la Mapinduzi na katika mazoezi yake huku
akiendelea kuwapa mbinu wachezaji katika kukijenga kikosi chake.
“Kabla ya mechi ya Azam FC, niliwakataza
viungo wangu kucheza pasi za nyuma wakati tukiwa na mpira, badala yake
kulishambulia goli la wapinzani wetu kwa kasi, lakini wenyewe walicheza pasi
nyingi za nyuma kitu ambacho sijawaelekeza, hali hiyo iliwapa Azam FC nafasi ya
kupumzika,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment