Uongozi wa Tawi la Mpira na Maendeleo maarufu
kama Simba Ukawa, umeibuka na kumtetea aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mzambia,
Patrick Phiri kuwa hakuwa na tatizo klabuni hapo.
Simba iliamua kuachana na Phiri baada ya kuona
mwenendo mbaya wa timu huku nafasi yake ikizibwa na Mserbia, Goran Kopunovic.
Katibu wa tawi
hilo, Mohamed Ally ‘Ngumi Jiwe’ alisema kumfukuza Phiri ni kosa kwani timu
ilikuwa katika hali nzuri lakini viongozi ndiyo waliokuwa wanasababisha matokeo
mabaya katika kila mechi.
“Tatizo ndani ya Simba si Phiri bali ni
uongozi, unamtolea nini kocha ambaye akifanya vizuri sawa lakini akiharibu moja
basi maneno mengi.
“Kama unakumbuka rais wetu Evans Aveva alisema
kuwa tatizo la Simba ni wachezaji ambao ni (Amri) Kiemba na (Haruna) Chanongo
lakini bado timu imeendelea kufanya vibaya,” alisema Ngumi Jiwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment