Michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea
huko visiwani Zanzibar imekuwa na kiingilio cha kima cha chini ambacho ni
shilingi 1,000 lakini kwenye mechi ya Simba kikaongezwa dau na kufikia shilingi
5,000.
Katika mechi zilizochezwa jana kati ya JKU na
Mafunzo majira ya saa 9 alasiri na iliyowakutanisha Polisi na Shaba iliyopigwa
saa 11 jioni, mashabiki waliingia kwa 1,000 lakini kwa staili ya kipekee.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza
mashabiki wote walitolewa nje na kisha kuanza kuingia tena kwa kiingilio
kingine kipya.
Halikadhalika ulipomalizika wa pili pia
mashabiki walifanya hivyo tena kwa ajili ya kuingia kuishuhudia Simba ikiumana
na Mtibwa majira ya saa 2.15.
Kutokana na ukubwa wa mechi hiyo mashabiki
walilazimika kulipa kiingilio cha shilingi 5,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment