January 3, 2015


Na Zaid Abdallah, Zanzibar
Simba imefanikiwa kuamka katika michuano ya Mapinduzi baada ya kuichapa Mafunzo kwa bao 1-0.


Simba imeibuka na ushindi katika mechi hiyo iliyoianza kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Shujaa wa Simba leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa ni Said Ndemla.

Ndemla alipiga shuti katika dakika ya 54 na kuzaa bao bilo. Ilikuwa ni baada ya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Kabla ya hapo, JKU iliing'ang'ania Mtibwa Sugar kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali uliochezwa mchana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic