Kocha Mkuu wa Yanga,
Mholanzi, Hans van Der Pluijm amesema atatumia Michuano ya Kombe la Mapinduzi
kukifanyia marekebisho kikosi chake kinachojiandaa na ligi kuu na Kombe la
Shirikisho.
Yanga inatarajiwa kuvaana na
BDF IX ya Botswana ambayo ni timu ya jeshi, Februari 13-15 mwaka huu, jijini
Dar na kurudiana kati ya Februari 27 na Machi Mosi, jijini Gaborone.
Pluijm amesema michuano hiyo itampa changamoto kwa kuwa pia
inashirikisha klabu kutoka nje ya Tanzania, hivyo anaamini ushindani utakuwa
mkubwa.
“Ni michuano mizuri kwa kuwa
tunakutana na timu kutoka nchi nyingine na wakati huohuo tutakuwa pamoja, hivyo
itakuwa rahisi kukifanyia marekebisho kikosi changu,” alisema Pluijm ambaye ni
mwanachama wa Yanga.
Timu kutoka nje ya Tanzania
ambayo inashiriki michuano hiyo ni KCC ya Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment