| WACHEZAJI WA SIMBA WAKISUJUDU BAADA YA MESSI (NAMBA 11) KUIFUNGIA SIMBA BAO HILO LILILOBAKI KUWA PEKEE KWENYE MECHI HIYO. |
Bao pekee la Messi, limeiwezesha Simba
kupata ushindi wa pili wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuishinda JKU.
Katika mechi hiyo ya Kombe la Mapinduzi
usiku huu, kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Simba ilipata bao lake kupitia
Ramadhani Singano ambaye zaidi anajulikana kama Messi.
Wachezaji wa Simba walionyesha soka safi
tokea kipindi cha kwanza, lakini JKU walionekana kutoa upinzani mkubwa.
JKU pia walionyesha kuwa na pumzi na stamina
ya kutosha hivyo kufanya watoe upinzani muda wote wa mchezo.
Hata hivyo, Simba hawakuwa makini kwani walionyesha
kuwa na mipangp mizuri ya kutengeneza nafasi, lakini tatizo likawa katika
umaliziaji.







0 COMMENTS:
Post a Comment