January 5, 2015


Baada ya kushinda mechi zake zote mbili za michuano ya Mapinduzi kwa mabao 4-0, kila moja, Yanga imeendelea na mazoezi ya kupasha misuli kuiwinda Shaba.


Yanga inashuka dimbani Amaan, Zanzibar kesho kuivaa Shaba katika mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi.

Mazoezi ya Yanga yalifanyika mjini hapa chini ya Kocha Hans van der Pluijm.

Hata hivyo hayakuwa mazoezi makali sana ikionyesha ni sehemu ya kuweka misuli safi kabla ya mechi hiyo ya kesho.

Yanga walishinda mechi zao mbili za kwanza wakianza kuitungua Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0 kabla ya kushinda kwa idadi hiyo katika mechi ya pili dhidi ya Polisi Zanzibar, jana.
Wakati Yanga itashuka dimbani saa 2 usiku kucheza na Shaba, Azam FC ndiyo itatangulia jioni kuwavaa Mtende, pia mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic