Mshambuliaji wa Simba, Danny Sserunkuma amesema timu za mikoani huzipania timu kubwa pamoja na wachezaji wa kimataifa.
Lakini amesisitiza hilo haliwezi kumzuia kutoa msaada kwa kikosi chake kwa kuwa anaamini Simba ina kikosi bora.
"Ukicheza mechi nje ya Dar es Salaam inaonyesha kuna ugumu maradufu. Hata Dar bado kuna ugumu pia kwa kuwa timu zinapania sana.
"Nafikiri wachezaji wa kigeni na timu kubwa pia zinaonekana ni sehemu ya changamoto kwa timu nyingine.
Sserunkuma ameanza kuonyesha cheche zake baada ya kufunga bao lake la kwanza la Ligi Kuu Bara akiwa ndiyo anacheza mechi yake ya pili ya ligi hiyo.
Mechi yake ya kwanza ilikuwa wakati Simba ilipoivaa Kagera Sugar na kulala kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.







0 COMMENTS:
Post a Comment