Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) litatuma waangalizi wa siri kwenye mechi za raundi ya 21
na 22 ambazo ni za mwisho kwa makundi yote ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
zitakazoanza kuchezwa Februari 10 mwaka huu.
Mwangalizi
huyo (match assessor) atatumwa na Katibu Mkuu ambapo baada ya mechi atatuma
ripoti kwake kwa hatua zaidi.
Mechi
za raundi ya 21 kundi A zitachezwa Februari 10 mwaka huu kati ya KMC na African
Lyon (Uwanja wa Mkwakwani), Kurugenzi FC na African Sports (Uwanja wa Mufindi),
Majimaji na JKT Mlale (Uwanja wa Majimaji), Kimondo FC na Friends Rangers (CCM
Vwawa, Mbozi), Ashanti United na Villa Squad (Uwanja wa Karume) na Polisi Dar
na Lipuli FC (Uwanja wa Azam Complex).
Raundi
ya 22 itachezwa Februari 16 mwaka huu kwa kuzikutanisha African Lyon na Polisi
Dar (Uwanja wa Karume), Kurugenzi na Lipuli FC (Uwanja wa Mufindi), Kimondo FC
na Majimaji (CCM Vwawa, Mbozi), JKT Mlale na Ashanti United (Uwanja wa
Majimaji), Friends Rangers na African Sports (Uwanja wa Taifa), na Villa Squad
na KMC (Uwanja wa Azam Complex).
Kundi
B raundi ya 21 ni Februari 17 mwaka huu kati ya Burkina Faso na JKT Kanembwa
(Uwanja wa Jamhuri), Mwadui na Polisi Tabora (Uwanja wa Mwadui), Polisi Dodoma
na Green Warriors (Uwanja wa Jamhuri), Rhino Rangers na JKT Oljoro (Ali Hassan
Mwinyi), Panone na Polisi Mara (Uwanja wa Ushirika), Geita Gold na Toto Africans
FC (Geita).
Februari
22 mwaka huu ni JKT Kanembwa na Green Warriors (Lake Tanganyika), Mwadui na
Burkina Faso (Mwadui), Polisi Tabora na JKT Oljoro (Ali Hassan Mwinyi), Polisi
Dodoma na Panone (Uwanja wa Jamhuri), Toto Africans na Rhino Rangers (CCM
Kirumba) na Geita Gold na Polisi Mara (Geita).
Mechi
za viporo za Polisi Mara zitachezwa Februri Mosi dhidi ya JKT Kanembwa, na
Februari 5 mwaka huu dhidi ya Polisi Tabora. Mechi zote zitachezwa kwenye
Uwanja wa Karume mjini Musoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment