Timu za
African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa
fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
African
Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa
kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya
Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa
kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B
ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.
Nazo timu za
Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika
nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka
Kundi A na Green Warriors Kundi B.








0 COMMENTS:
Post a Comment