| KOCHA MKUU WA TOTO, JOHN TEGETE NA KIKOSI CHAKE. |
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salamu za
pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji
(Ruvuma), Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu zao
kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Katika
salamu zake Bw. Malinzi amesema vilabu hivyo vinapaswa kujipanga na kufanya
maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL
ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo
mazuri kuepeuka kushuka daraja.
Kwa niaba
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF, familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto
Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL
2015/2016.







0 COMMENTS:
Post a Comment