Azam FC wameahidi kupambana hadi kieleweke licha ya mbwembwe za kutaka kuwachanganya kutoka kwa wapinzani wao El Merreikh.
Tayari Azam FC, wako mjini Kharthoum, Sudan wakisubiri mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa keshokutwa Jumamosi.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara, waliinyoa El Merreikh kwa mabao 2-0 jijini Dar.
Meneja wa Azam FC, Jemedari Said amesema wanajua kwamba wapinzani wao wamekuwa wakijitahidi kuwakoroga ili washindwe kucheza vizuri.
"El Merreikh ni wazoefu wa michuano ya kimataifa, wamekuwa wakifanya kila linalowezekana kutuvuruga kuanzia nje ya uwanja.
"Sisi tunaona hiyo hali, tunajua wanafanya nini na si mara ya kwanza wao kuanza kufanya hivyo. Hivyo haitupi shida.
"Hatuwezi kusema tunaichukulia mechi hiyo juujuu, lakini nakuhakikishia tutapambana na kila mmoja kati yetu analijua hilo," alisema.
Azam FC ndiyo mara ya kwanza inacheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ilianza kwa kuifunga timu kongwe barani Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment