February 26, 2015


Wanachama na baadhi ya mashabiki wa Yanga wameondoka jijini Dar es Salaam kwenda Botswana kuipa nguvu timu yao ambayo inapambana kuing’oa BDF XI katika michuano ya Kombe la Shirikisho.


Mashabiki hao wamepitia mpaka wa Tunduma nchini Tanzania hata hivyo wamelazimika kusafiri na basi dogo aina ya Toyota Costa wakiliacha jijini Dar es Salaam lile kubwa aina ya Yutong ili kukwepa gharama.

Watu  50 walitakiwa kulipa nauli ili kulitumia basi hilo kuja hapa Botswana lakini ikashindikana kutokana na wachache tu wapatao 15 kufanya hivyo.

“Kweli basi limebaki Dar es Salaam. Mashabiki wanakuja na Costa na tumewasiliana nao leo asubuhi wamesema wameshavuka Tunduma. Tunatarajia watafika hapa usiku wa leo na kesho tutakuwa nao kwenye mechi,” alisema Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro.

Yanga ipo mjini hapa na mashabiki kadhaa wa BDF wamekuwa wakizungumza kuhusiana na ujio wa timu hiyo jijini hapa, huku baadhi wakijipanga kusafiri hadi Lobatse, kilomita 70 kutoka hapa ili kwenda kuishuhudia mechi hiyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic