BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA WAKIWA KWENYE UWANJA WA LOBATSE NCHINI BOTSWANA IKIWA NI BAADA YA KUMALIZA MAZOEZI, LEO. |
Uongozi wa Yanga umesema umeukubali Uwanja
wa Lobatse kwamba uko safi na unastahili kuchezewa pambano la kimataifa.
Yanga inashuka dimbani kwenye Uwanja wa
Lobatse mjini Lobatse kuivaa BDF
katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho, kesho.
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema uwanja
huo una vigezo vyote na wanaamini watacheza vizuri.
“Ni uwanja mzuri na wote tumeuona, baada ya
mazoezi kila kitu kimekwenda vizuri na kila mmoja wetu ameridhika na uwanja.
“Hatuwezi kuwa malalamiko yoyote kuhusu
uwanja, hadi sasa tunachosubiri ni mechi tu,” alisema.
Uwanja wa Lobatse, uko kilomita 70 kutoka
jijini Gaborone ambao ni mji mkubwa kuliko yote nchini Botswana.
0 COMMENTS:
Post a Comment