February 4, 2015


Baada ya kufanikiwa kufumania nyavu kwa mara ya kwanza, straika mahiri wa Polisi Moro, Said Bahanuzi, amefungua kinywa na kusema kuwa amefurahi sana kuipa heshima klabu yake mbele ya Mbeya City.

Timu hizo zilikutana wikiendi iliyopita katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Morogoro, ambapo Polisi Moro iliilaza Mbeya City kwa bao 1-0.

Bahanuzi amesema kuwa amefurahi kufunga bao hilo pekee katika mchezo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu, hivyo atahakikisha anafanya jitihada za kuendelea kuisapoti timu hiyo.

“Mchezo ulikuwa mgumu sana, kikubwa namshukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kufunga bao moja tena la pekee mbele ya wapinzani wetu Mbeya City, naamini hiyo ni heshima tosha kwa upande wangu.


“Msimu huu ligi ni ngumu sana tofauti na miaka ya nyuma, lakini nitahakikisha natoa mchango wangu wa hali na mali ili kuinusuru timu yetu katika panga la kushuka daraja,” alisema Bahanuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic