Klabu ya Barcelona imeonyesha
heshima kubwa kwa kuupa uwanja wake wa mazoezi wa timu kubwa jina la 'Camp Tito
Vilanova'.
Klabu hiyo imeamua kufanya
hivyo ikiwa ni heshima kwa aliyekuwa kocha wake, Tito Vilanova aliyefariki
dunia mwaka jana kutokana na ugonjwa wa kansa.
![]() |
| VILANOVA (KULIA) WAKATI WA UHAI WAKE ALIPOKUWA KOCHA MSAIDIZI CHINI YA PEP GUARDIOLA. |
Wachezaji wote, viongozi
pamoja na familia ya Vilanova walikuwa uwanjani hapo wakati wa shughuli hizo za
kutangaza jina hilo rasmi.










0 COMMENTS:
Post a Comment