February 26, 2015


Daudi Hamis, Gaborone
Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi kwenye Uwanja wa Lobatse ikiwa ni siku moja kabla ya kuwavaa BDF XI.


Yanga inaovaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa kesho saa 1:30 kwa saa za hapa na saa 2:30 kwa saa za Afrika Mashariki imemaliza mazoezi yake vizuri kabisa.

Wachezaji walifika asubuhi katika Uwanja wa Lobatse na kuanza kufanya mazoezi, lakini kabla ya hapo, Kocha Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Boniface Mkwasa waliukagua uwanja huo.

Yanga ilifanya mazoezi mepesi na baadaye wachezaji waligongeana mpira ikiwa ni sehemu ya kupasha viungo.

Jana, Yanga walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Jeshi katika jiji hili.

Kutoka Gaborone hadi Lobatse ni kilomita 70.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic