HII ILIKUWA NI GAME YA MWISHO ANFIELD, MSIMU ULIOPITA, LIVERPOOL IKIWA NA SUAREZ. MECHI YA KESHO CITY WANAKWENDA TENA ANFIELD WAKIWA WANAUTAKA UBINGWA TENA. |
Manchester City wanashuka dimbani kesho kuwavaa Liverpool katika mechi ya Ligi Kuu ya England wakijua ndiyo kombe pekee wanaloliwania pia wanalopaswa kulitetea.
Hawamo Capital One, FA na Ligi ya Mabingwa mwendo wao hauna uhakika. Sasa wataifunga Liverpool kesho ambayo katika mechi tano walizokutana nayo wameifunga mara 2, imewafunga mara moja na sare 2?
Liverpool ina majeraha ya kung'olewa kwenye Kombe la Europa, itakubali kilahisi tena ikiwa nyumbani?
City walifungwa mabao 2-1 na Barcelona kwenye
hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki hii, wameshatolewa
kwenye Kombe la FA pamoja na Capital One hali ambayo itawafanya wafanye kazi ya
ziada ili waweze kumaliza msimu na kombe.
Watatakiwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi
ili waweze kupunguza gepu kati yao na vinara Chelsea na kubakiza pointi mbili,
kwani sasa wanadaiwa pointi tano wakiwa nafasi ya pili.
Pamoja na kwamba wana kikosi cha bei ghali,
City walimaliza michezo minne bila kupata ushindi hivi karibuni ambapo kiungo
wao mahiri, Yaya Toure, alikuwa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
(Afcon).
Lakini kitendo chao cha kuanza kupata ushindi
dhidi ya Stoke City na Newcastle United, kimewafanya kuanza kurejea kwenye kasi
yao.
Hali hii inawafanya waaminike kuwa, wanaweza
kufanya maajabu kesho na kuifanya Chelsea ya Mourinho kuanza kuweweseka.
Lakini kazi haitakuwa ndogo wakati unapocheza na
timu ngumu kama Liverpool ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kati ya 10 ya
hivi karibuni kwenye Ligi Kuu ya England.
Mchezo wa kesho unasubiriwa kwa hamu kubwa na
mashabiki kwenye Uwanja wa Anfield kutokana na kiwango cha timu yao cha hivi
karibuni.
Kwa mara ya kwanza, Liverpool walipoteza dhidi
ya Manchester United, Desemba 14, mwaka jana ilipokula kichapo cha mabao 3-0 na
kusogea hadi katikati ya msimamo wa ligi hiyo.
Mashabiki wanaamini kuwa ushindi wa hapa
utawafanya Liverpool kuwa na matumaini makubwa ya kumaliza msimu huu wakiwa katika
nafasi nne za juu.
Liverpool ambao kwa sasa wapo nafasi ya sita, wamefanikiwa
kushinda michezo miwili migumu ya hivi karibuni dhidi ya Southampton walipopata
ushindi wa mabao 2-0, lakini pia wakiwa wamewachapa Spurs mabao 3-2 na sasa
wapo pointi tatu tu nyuma ya Arsenal waliopo nafasi ya tatu.
Mastaa wa Liverpool, Philippe Coutinho, Raheem
Sterling na Daniel Sturridge, wamekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu sana kwa
kipindi cha hivi karibuni, jambo ambalo ni hatari sana kwa City.
Lakini bado kila mmoja anafahamu kuwa City ni
timu hatari ikiwa na wanaume kama Yaya, Sergio Aguero na David Silva ambao
wamekuwa wakifanya maajabu sana msimu huu.
Mwamuzi:
Mwamuzi wa mchezo huu ni Mark Clattenburg,
mwamuzi huyu amekuwa na majanga ya hapa na pale, lakini akiwa bora sana wa
kutoa kadi nyekundu uwanjani.
Ni mmoja kati ya waamuzi bora kwenye Ligi Kuu
England lakini karibu kila msimu amekuwa akikumbana na majanga, mwanzoni mwa
msimu huu alisimamishwa baada ya kupanda gari binafsi wakati akitoka kwenye
mchezo kati ya West Brom dhidi ya Crystal Palace ili kuwahi kwenye pati jijini
Newcastle.
Uso
kwa uso:
Man City 3 - 1 Liverpool
Liverpool 3 - 2 Man City
Man City 2 - 1 Liverpool
Man City 2 - 2 Liverpool
Liverpool 2 - 2 Man
City
0 COMMENTS:
Post a Comment