Kesho itakuwa siku nyingine ya kujiuliza maswali kwa Arsene Wenger wakati kikosi chake cha Arsenal kitakaposhuka dimba katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu England.
Arsenal vs Everton
Baada ya kula kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa
AS Monaco, Arsenal watarejea tena kwenye Uwanja wa Emirates, kesho wakitarajia kufanya
maajabu kwenye Ligi Kuu ya England.
Vijana wa Kocha Wenger, wanaweza
kupata mapokezi mabaya kutokana na kiwango kibovu ambacho walionyesha kwenye
mechi hiyo ya Jumatano iliyopita.
Ushindi tu ndiyo unaweza kuwafanya wakaendelea
kuwa na kasi nzuri, kwani wanaonekana kupishana kwa pointi tatu tu na Liverpool
ambao wapo nafasi ya sita.
Arsenal wanafahamu kuwa pamoja na kwamba
Everton msimu huu wanasuasua, bado wanaweza kufanya maajabu kama walivyofanya
kwenye mchezo wa kwanza ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Katika mchezo huo, Arsenal walilazimika
kusawazisha baada ya kutanguliwa hali ambayo inaweza kuwapa hofu kubwa vijana
hao wa London hiyo kesho.
Arsenal wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye
michezo kadhaa iliyopita ambapo wameweza kutoka katika nafasi ya saba hadi
kutua kwenye tatu bora.
Everton kwa sasa wapo katika nafasi ya 12,
wakiwa wameshinda mechi sita tu kati ya 26 na wanajua kuwa kupoteza mchezo wa
leo ni jambo baya sana kwao na wakati wowote wanaweza kusogelea kwenye mstari
wa kushuka daraja.
Taarifa zinasema kuwa huu unaweza kuwa mchezo wa
mwisho kwa kocha wa timu hiyo, Roberto Martinez, endapo watapoteza.
Uso kwa uso
2014/2015 : Everton 2 - 2 Arsenal
2013/2014: Everton 3 – 0 Arsenal
2013/2014: Arsenal 4 – 1 Everton
0 COMMENTS:
Post a Comment