February 24, 2015

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI.

Kamati ya Utendaji ya Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokutana Jumapili Februari 22 mwaka huu, imefanya mabadiliko ya mahali utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka Mkoa wa Sinigida na kuhamishia mkoa wa Morogoro.


Hatua hiyo imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo ka shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.

Kamati ya Utendaji inamshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida (Sirefa), na uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza kuandaa mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.


TFF itaandaa vikao na matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadae, tarehe ya mkutano mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic