February 25, 2015


Klabu ya Simba isipokuwa makini katika kuwaongezea wachezaji wake 11 mikataba, basi huenda ikawapoteza nyota 11 ambao wengi wao ni tegemeo kwenye kikosi cha Mserbia, Goran Kopunovic.


Simba imeonekana kusuasua msimu huu lakini pia ina hali ngumu kwa kuwa wachezaji wake 11 wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu.

Simba inaweza kuwapotezea wachezaji wao kwenye kikosi cha Yanga ambacho kimekuwa kikiwawinda baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kwa kipindi tofauti.

Wachezaji hao ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika ni Ivo Mapunda, Said Nassor ‘Chollo’, Joseph Owino, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Said Ndemla na Haroun Chanongo.

Wengine ni Shaaban Kisiga, Adam Miraji, Abdallah Seseme, Hassani Isihaka na William Lucian ‘Gallas’ ambao wote hivi sasa wanaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kuwa wamebakiza chini ya miezi sita.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, kamati ya usajili ya timu hiyo, tayari imeanza mazungumzo ya awali na baadhi ya wachezaji wanaowahitaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

Chanzo hicho kilisema, uongozi utawabakiza wachezaji hao wanaowataka baada ya kumtathmini kila mmoja kulingana na mchango wake katika timu na mahitaji ya kocha wao.

 “Nusu ya wachezaji kiukweli mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini uongozi umefanya mazungumzo ya awali na baadhi ya wachezaji wale muhimu tunaowahitaji kwa ajili ya msimu ujao.


“Kikubwa tumepanga kukiimarisha kikosi chetu kwa kuziboresha baadhi ya nafasi, tayari uongozi umefanya tathmini ya kila mchezaji kwa kuangalia kiwango chake kabla ya kumsajili,”  kilisema chanzo hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic