Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm ambaye baadhi ya wachambuzi waliwahi kumponda na kudai hana lolote, eti ana umri mkubwa, sasa ameonyesha anaweza.
Licha ya kikosi chake kucheza vizuri, Mholanzi huyo ameacha rekodi ya pekee jijini Mbeya wakati alipokuwa akikiongoza kikosi chake
katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons na Mbeya City.
Katika mechi hizo, Yanga ilifanikiwa kuibuka na
ushindi ambapo iliitandika Prisons mabao 3-0 na baadaye ikiinyuka Mbeya City
mabao 3-1 na kufanikiwa kuondoka jijini humo.
Mechi hizo zimeifanya Yanga ikusanye pointi
sita kwenye mechi mbili ugenini.
Rekodi ambayo Pluijm ameiacha jijini Mbeya ni
ile ya kuiwezesha Yanga kuibuka na pointi sita jijini hapo kwa mara ya kwanza
tangu mkoa huo uwe na timu mbili za ligi kuu.
Misimu mingine Yanga imekuwa ikiambulia pointi
tatu au moja na kuna wakati mwingine ilikuwa ikiondoka patupu mkoani humo bila
ya ushindi wa aina yoyote.
Hali hiyo ilimfanya Pluijm pamoja na baadhi ya
viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo kushangilia kwa furaha ya ajabu baada
ya kumalizika kwa mechi yao ya mwisho dhidi ya Mbeya City.
Mara ya mwisho Yanga ilishinda mkoani Mbeya zaidi ya miaka minne iliyopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment