Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la
COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la vyama vya soka Kusini
mwa Afrika (Cosafa).
Michuano
ya kombe la Cosafa inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka
huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa
kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa
moja na kituo cha Luninga cha Supersport 4.
Taifa
Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane
zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya
robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho,
Madagascar, Marutius, Namibia, Shelisheli, Swaziland.
Katika
kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi
ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi
za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo
zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango
vya FIFA.
Kombe
la Cosafa lilianzishwa mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa
Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo
Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi
wanachama wa Cosafa ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros, Lesotho,
Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji,Namibia, Reunion, Sychelles,
Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment