Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars),
Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini, kitakachoingia
kambini siku ya Jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya
Zambia mwezi Machi mwaka huu.
Kaijage ametangaza program yake ya mazoezi itakayochukua
takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya
mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza
mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa
awali.
Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imeingia moja kwa moja katika hatua ya
pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa
viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma
Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma
Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu,
Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia
Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai
Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa
Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.








0 COMMENTS:
Post a Comment