February 26, 2015


Mashabiki wa soka wakiwemo Watanzania na raia wa Kenya na Uganda wameungana kuishangilia Yanga ambayo iko jijini hapa kuivaa BDF XI ya Botswana.


Yanga inaovaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa leo saa 1:30 kwa saa za hapa na saa 2:30 kwa saa za Afrika Mashariki.

Katika mitaa mbalimbali ya jiji hili, mashabiki wa nchi hizo tatu wameungana na kuishangilia Yanga wakionyesha kudumisha umoja wa Afrika Mashariki.

Ingawa si wengi, jana mchana mashabiki hao wamekiwemo wanafunzi walikuwa wakipanga namna ya kufanya ili kupata usafiri wa uhakika utakaowapeleka Lobatse kwenda kuishangilia Yanga.

Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema mashabiki hao, hasa wale wa Tanzania wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu.

Botswana ni kati ya nchi Kusini mwa bara la Afrika ambayo Watanzania wengi wanaishi wakiwa wanafanya biashara zao na wengine wakiwa wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya jiji hili na katika mikoa mingine.


Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 katika mechi yake ya kwanza jijini Dar es Salaam na BDF imepania kushinda na kusonga mbele katika mechi ya leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic