February 24, 2015


Kiungo Andrey Coutinho analazimika kubaki jijini Dar es Salaam wakati Yanga inatarajia kuondoka na kikosi cha watu 20 kwenda nchini Botswana, kesho.


Coutinho raia wa Brazil amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika siku za hivi karibuni na kupewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Yanga inakwenda kuivaa BDF XI ya nchini humo katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho. Katika mechi ya kwanza Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 jijini Dar.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema Coutinho bado hajawa fiti baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Mbeya City mjini Mbeya.

"Wachezaji watakaokwenda ni ishirini na Coutinho ni kati ya wale watakaobaki," alisema Pluijm.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic