Kocha Carlo Ancelotti anaonekana ameanza
kukitengeneza kikosi chake kisaikolojia kabla ya mechi ya El Clasico dhidi ya
Barcelona, Jumapili.
Ancelotti aliamua kuingia mfukoni na kutoa
fedha zake kuwapeleka wachezaji wake kula chakula cha usiku kwa pamoja.
Inaonekana amelenga kuwafanya wajione wapo
pamoja kamafamilia.
Madrid wanakutana na Barcelona wakiwa
wanatoka katika hali ya kuhangaika na kiwango chao si bpra.
Wakati Barcelona iko katika kiwango kizuri na hasa mshambuliaji wake, Lionel Messi.








0 COMMENTS:
Post a Comment